TATIZO LA STROCK (KUPOOZA VIUNGO)
JE! UNAIFAHAMU STROKE? Stroke ama ugonjwa wa kupooza ni tatizo linalowasumbua watu wengi zaid duniani lakini wengi wetu hawajui chanzo cha ugonjwa huo. Chanzo kikubwa cha stroke ni kuziba, kuvuja ama kupasuka kwa mirija ya damu katika kichwa. Nini chanzo cha tatizo hili? Chanzo cha tatizo hili ni matumizi ya mafuta ya wanyama ambayo kiasili yana uwezo wa kuganda (colestral). Mafuta haya yakishaingia mwilini yanaganda katika mishipa ya damu na kupunguza ukubwa wa mishipa hiyo, hapo utaanza kupata presha ya kupanda HBP kwa kuwa mishipa hiyo itakuwa imepungua kipenyo chake na damu italazimika kupenya kidogo licha ya kuwa inasukumwa kwa Kasi ile ile. Katika mazingira hayo inaweza kutokea kipande cha mafuta yaliyoganda kikameguka na kusafiri katika mishipa pamoja na damu. Safari hiyo inaenda kukwamia katika mishipa ya kichwa ambayo ni madogo zaidi. Kipande hicho kinaziba kabisa mshipa huo na kusababisha damu usiweze kufika katika baadhi ya viungo, hapo ndipo stroke inaponza. Iwap...